>Sasa yani ndio nimemaliza leo chuo alafu jamaa wanataka watu wenye experience, duuh! hii sio sawa
Mimi naona ipo sawa na wala sio kwamba system inatuonea,
Point yangu itaeleweka vizuri kama tukielewa mzizi wa hili, na nimekuja kuona kwenye mzizi hapo hapo pia ndio kwenye upenyo wa kututoa kama magraduate kwenye hii system.
Tukiangalia kwa jicho la mfanyabiashara(mwajiri):
Nataka kila siku nipate faida (tena kwa speed).
Haya tuamishie jicho kwenye vitu tunavyofundishwa chuoni:
Vipo general, haufundishwi utakavyoenda kufanya kazini.
Unajifunza utakavyofanya kazini KAZINI.
Sasa kwa hili kama mfanyabishara, ni hasara:
Nataka ukifika kazini leo, uje tuendeleze marathon, tena ikiwezekana uje na makubwa ili tuzidi kupata faida.
Maana ya hapa ni kwamba nataka mtu ambaye tayari ameshapata shule ya kazini (experience).
Sasa wewe kwa sasa “hujui” kitu kwa hiyo kukuchukua mpaka tupige hesabu za kiuchumi kwanza (je sipati hasara sana?)
Okay upenyo wetu uko wapi?
Siwezi kukupigisha hasara.
Ndio. Huu ndio upenyo tunaoweza kupitia kama hivi:
1.Vitu “general” nilivyofunzwa chuoni nimevielewa vizuri kutengeneza skills ambazo naweza kuadapt mapema kwa kitu chochote nitakachokutana nacho kazini.
2.Usinione hivi tu kuna vitu naweza fanya kazini kwako ukapata faida ambazo hukutegemea
Yeah, naweza kuongea hivi kwenye interview au kwa yoyote atakayeingia kwenye anga zangu, lakini namna bora ni mtu kuweza ku “feel” kweli upo hivyo, na hii itawezekana tu kwa yeye kuweza kujua vitu vyote nilivyoweza kufanya mpaka sasa:
Project nilizofanya, wakati nilipojitoa kwa ajili ya kutatua changamoto walizokuwa nazo watu, kampuni au taasisi(bila kuambiwa na kutaka kulipwa), ujuzi special niliojifunza, nafasi za uongozi nilizoshika,
list ipo kubwa na vingine sivijui ila unaweza ongezea hapo chochote ulichoweza kufanya na unachofanya asaivi ambacho kitamfanya mtu kusema “huyu kijana anatufaa sana, nawezaje kumpata?”
In short tunachokifanya hapa nikumrudishia mpira mwajiri kwa kumwonesha tunaweza kumpa kitu anachokihitaji zaidi:
Faida inayoongezeka kila siku kwa speed.
Na anayetupa huo mpira ni wewe.
Swali linakuja, vitu gani unafanya asaivi kukupa hiyo elimu ya kazini ukiwa bado chuoni?
Hivi ndivyo vitavunja kigezo cha experience ya miaka kazaa ili uweze kupata ajira mapema.
#risefromCollege huo ndio upenyo wako.
Kama unashahuku kujua namna ngani unaweza anzisha safari yako ya mafanikio ukiwa chuoni, unaweza anzia kusoma hapa. #moreExposure #buildUpSkills #TryOutThings